Sporting CP inaanza kampeni yake ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuikaribisha Galatasaray katika Uwanja wa José Alvalade Inchini Ureno. Mchezo huo utapigwa leo Jumatano, saa 22:00 usiku.
Huu ukiwa ni moja ya michezo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa katika raundi ya kwanza ya hatua ya ligi. Sporting itakuwa na faida ya kucheza nyumbani, huku Galatasaray ikitafuta matokeo mazuri ugenini.
Sporting CP inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na matumaini makubwa kutokana na uwezo wake wa kucheza vizuri mbele ya mashabiki wake. Timu hiyo ya Ureno inatarajiwa kutumia kasi ya kushambulia, presha ya juu na mipira ya pembeni kujaribu kuivuruga safu ya ulinzi ya Galatasaray. Kwa upande wao, nidhamu ya safu ya nyuma itakuwa muhimu ili wasiruhusu wageni kutumia nafasi zitakazojitokeza katika mashambulizi ya kushtukiza.
Galatasaray, chini ya kocha Okan Buruk, ina uzoefu wa michezo mikubwa ya Ulaya na haitarajiwi kwenda Lisbon kwa ajili ya kujilinda pekee. Kikosi hicho cha Uturuki kinaweza kutegemea nguvu yake katika kushambulia kwa haraka mara baada ya kuupata mpira. Changamoto yao kubwa itakuwa kuhimili presha ya Sporting na kuhakikisha hawapotezi umiliki wa mpira katika maeneo hatari.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kimbinu, vita kubwa inaweza kuonekana katikati ya uwanja. Sporting itataka kutawala mchezo na kuwalazimisha wageni kurudi nyuma, wakati Galatasaray inaweza kusubiri nafasi ya kuvamia nafasi zitakazoachwa na wenyeji wanapopanda.
Takwimu za kabla ya mchezo zinaipa Sporting nafasi nzuri zaidi kutokana na faida ya nyumbani, lakini pengo hilo si kubwa kiasi cha kuifanya Galatasaray ionekane haina nafasi.
Kwa ujumla, huu ni mchezo unaoweza kuamua mambo kupitia umakini, matumizi ya nafasi na uwezo wa timu kuvumilia presha. Sporting CP inaonekana kuwa na faida kutokana na kucheza nyumbani, lakini Galatasaray ina uzoefu wa kutosha kuifanya mechi kuwa ngumu.