Screenshot
SIMA Constantine, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa nchini Tanzania (ALAT), Sima Constantine, amelaani vikali mauaji ya diwani wa Kata ya Misechele, wilayani Tundulu mkono Ruvuma (CCM), Zuberi Abas Binam. Anaripoti Sadam Zinga, Mwanza … (endelea).
Mauaji dhidi ya diwani huyo, yamefanyika 16 Oktoba mwaka huu, wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Sima smesema, diwani huyo ameuawa baada ya kuvamiwa na kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji.
Ameiomba Serikali kupitia uongozi wa mkoa wa Ruvuma na wilaya ya Tunduru, kuchukua hatua stahiki za kiusalama, kuhakikisha waliohusika na tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka.
Mwenyekiti huyo wa ALT amesisitiza umuhimu wa vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini waliohusika na kuhakikisha wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Katika muda sasa, wilaya ya Tunduru imekumbwa na mfululizo wa mapigano baina ya wakulima na wafugaji, yaliyosababisha vifo, majeruhi, ulemavu, uharibifu wa mali pamoja na miundombinu ya umma.
Wakati hayo yakiendelea, Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma, limetangaza kuwashikilia watu 15 kutoka jamii ya wafugaji, kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu wawili na kujeruhi wengine watatu katika Kitongoji cha Mkambala, Wilaya ya Tunduru.
Waliofariki katika shambulio hilo lililotokea usiku wa 16 Oktoba 2026, ni pamoja na diwani huyu wa Kata ya Misechela (51) na mfanyabiashara Omari Zuberi Yassini (45).
Majeruhi watatu wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Tunduru.
MwanaHALISI ONLINE limebaini kuwa mauaji hayo, yalitokana na mfululizo wa mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyoanza baada ya mkulima mmoja kuchomwa mkuki na wafugaji, hatua iliyosababisha wanakijiji kuvamia makambi ya wafugaji na kumjeruhi mtoto wa miaka 12.