KLABU ya soka ya Yanga kwa kushirikiana na Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL), wamezindua msimu wa tatu Safari Lager Cup ambapo wanasaka vipaji vya soka nchini.Anaripoti Mwandishi wetu , Dar es Salaam … (endelea).
Uzinduzi huo umefanyika leo, tarehe 5 Oktoba 2026 katika Uwanja wa KMC na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa TBL nchini, Michelle Kilpin amesema wanaanza safari nyingine ya kukuza soka kwa kusaka vipaji ambavyo havijaonekana ili vionekane na kuendelezwa.
Amesema kampuni yake imekuwa ikifanya vizuri katika sekta ya michezo ambapo kwa muda mrefu wanaendesha mashindano ya Kilimanjaro Marathon
Katika misimu miwili ya Safari Lager Cup wamepata mafanikio makubwa na wanatarajia msimu wa tatu uende mbali zaidi na kuwafikia vijana wengi kwa kushirikiana na watu mbalimbali.
“TTF wametusaidia msaada wa utaalamu na watu mbalimbali. Yanga nao wametusaidia kuwapa fursa vijana tunaowapata na tunaamini watafika mbali” amesema.
“Tunaamini jitihada hizi na za wadau tofauti zitasaidia kwenda mbele na tunajua huko kwenye jamii kuna vipaji vinahitaji kuonekana, vinatusubiri sisi tuvifikie na kuviibua”
Kensan Mkhombo-Mkurugenzi wa Masoko TBL, amesema wana miaka mitatu sasa na wnajivunia kuwa Safari Lager Cup imeleta mabadiliko makubwa ya kisoka hapa nchini.
“Yanga wametusaidia kukuza vipaji vya vijana, tunawaomba Watanzania wote tushirikiane kuhakikisha vipaji vinaibuliwa na kubadilisha maisha ya vijana wetu” amesema.
Andre Mtine, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa klabu ya Yanga amesema ushirikiano wao na TBL wetu na Safari unatoa fursa ya kukuza vipaji.
Amesema kuwa wanaamini kurudisha mpira kwa jamii kunawezesha vipaji kukua na soka kuendelea kuanzia ngazi za chini.
“Kuna vipaji vingi sana mtaani vinavyohitaji kuibuliwa, tunaamini katika nguvu ya vijana na tunaamini kwao katika maendeleo ya soka letu,” amesema.
Amesema kuwa katika awamu ya pili walipata mchezaji mmoja na ninaamini awamu ya tatu itakuwa na mafanikio makubwa zaidi”
Charles Maguzu- afisa michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), amesema Safari Lager Cup awamu ya tatu itasaidia kufikia vipaji vingi vya vijana wanaocheza mpira wa miguu.
“Naamini vijana wataopatikana watafanya vizuri kitaifa na kimataifa.
Matokeo ya kunyanyua vijana ni kufanya taifa kuwa na tibu bora za kitaifa na kimataifa.”
“Ushirikiano wa kila.mdau katika sekta ya michezo utawezesha vipaji vya watu kukua na taifa kupiga hatua zaidi.” Amesema
Amewaomba wadau wengine wajitokeze katika kusaka vipaji vya michezo mbalimbali hapa nchini.
“BMT tutashirikiana na kila mmoja wetu kufikia malengo yaliyokusudia”
Naye Pamela kutoka TBL anayeshughulika na kusaka vipaji, amesema wanachozingatia mwenye nidhamu, kipaji na bidii kufanikiwa atapata fursa ya kuchukuliwa na Yanga baada ya kuletwa na safari.
“Watanzania wanaruhusiwa kupicha video na kuituma kwa timu ya safari ambapo watachukuliwa kwenye mabonanza mbalimbali. Tunataka wenye miaka 18 hadi 23 wanaruhusiwa kujisajili.
Amesema wataendesha mabonanza ya kusaka vipaji kwa kanda (mikoa minne) ambapo wataanza mkoani Mbeya tarehe 24 Oktoba 2026 kupitia ofisi za TFF ndizo zitahusika.
Mwanza tarehe 7 Novemba 2026, tarehe 21 Novemba 2026 mkoani Arusha na Dar es Salaam, itakuwa ni tarehe 5 Desemba 2026
Nao wachezaji walionufaika na programu hiyo Selemani Agustino (Mangoma) na
Lupasisyo Abraham wamesema miongoni mwa mafaniko waliyopata ni kucheza ligi daraja la pili Zanzibar na kufanya majaribio katika klabu.
Mwisho.
Habari za kazi. Naomba kufahamu kuhusu mashindano ya Safari Lager Cup yanayolenga kusaka vipaji vya soka Tanzania. Mimi ni kijana mwenye ndoto ya kuwa mchezaji wa kulipwa, na ningependa kushiriki mashindano haya. Je, kuna njia ya kujisajili online au kutuma video yangu ya kucheza mpira? Naomba mnisaidie kupata maelekezo rasmi ya usajili. Asanteni.
taratibu za Usajili zipo kwenye vituo pekee ambavyo ni Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza