IMEELEZWA kuwa Boniface Mwabukusi, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amehojiwa na jeshi la polisi kuhusu tuhuma za kufadhili maandamano ya Oktoba 29 mwaka huu.Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo yameelezwa leo tarehe 15 Oktoba 2026, na Jebra Kambole aliyekwenda naye katika kituo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam (Central), ambaye ameeleza kuwa Mwabukusi amehojiwa kama shahidi na sio mtuhumiwa.
Jebra amesema kuwa mahojiano hayo yaliyodumu kwa takribani saa tatu kutoka saa 3 asubuhi mpaka mchana alihojiwa kuhusu baraza la uongozi la TLS kupekea fedha kwa ajili ya kufadhili maandamano ya Oktoba 29 mwaka huu.
Tarehe 29 Oktoba mwaka jana wakati wa Uchaguzi Mkuu kuliibuka maandamano yanayoitwa Vurugu zilizokusudia kupindua serikali zilipelekea hasara na mauaji ya watu 518.
Kwa mujibu wa Jebra Mwabukusi aliwajibu polisi kuwa akaunti za TSL ziko wazi hakuna pesa yoyote iliyoingia kwa ajili ya kufadhili maandamano hayo.
Katika tuhuma nyingine Mwabukusi aliyohojiwa anadaiwa kuwa kufadhili vijana kwenda nchini Kenya ili kupata mafunzo ili kujiandaa na vurugu .
Pamoja na tuhuma hiyo imedaiwa kuwa TSL chini ya uongozi wa Mwabukusi imeacha shughuli zake inafanya harakati.
Mwabukusi amejibu kuwa TLS inafanya harakati za kitaaluma kwa lengo jema kwa taifa ikiwa pamoja na kusimamia kifungu cha 4 ya sheria ya kuundwa kwake.
Pamoja na hayo Ameonesha video mbalimbali ikiwemo mambo ya DP world amesema yeye kaka Rais wa TL ametimiza wajibu wake.Ameeleza mbele ya jeshi la polisi kwamba TLS inafanya mambo yake kisheria.
Pamoja na hayo yote aliachiwa kwa kudhaminiwa na sisi mawakili wake kwa sharti siku atakayoitwa aende.