ALIYEKUWA Waziri wa Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, katika Serikali ya Rais John Magufuli, Luhaga Mpina amesema, hata Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akiwa Makamu wa Rais kwenye serikali ya mtangulizi wake, alikuwa na migogoro mikubwa, “lakini hapakutumika ujanjaujanja ili ajiuzulu.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mpina akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 15 Oktoba 2026, jijini Dar es Salaam amesema, kuwa pamoja na kutokuwepo kwa maelewano kwa viongozi hao wawili, lakini hawakufikia kumtaka mmoja ajiuzulu.
Mpina amesema kuwa hayo yametokana kutokana na mchakato wa katiba ulivyokuwa mgumu kwa Makamo wa Rais kujiuzulu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo tarehe 15 Oktoba 2026, Mpina amesema, “…hata Rais Samia alikuwa na mgogoro mkubwa na Magufuli, lakini hapakuwapo hila zilizosababisha yeye kujiuzulu.”
Aliyekuwa mgombea urais wa chama cha ACT- Wazalendo atika uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba mwaka jana na baadaye kuenguliwa na Tume ya Uchaguzi, amedai kuwa Magufuli na Samia, walikuwa kwenye mgogoro mkubwa, lakini mtangulizi wake huyo, hakufika mahali kumlazimisha makamu wake kuondoka madarakani.
Hata hivyo, gazeti hili limeshindwa kumpata msemaji wa Ikulu, kuthibitisha madai ya Mpina, hadi taarifa hii inachapishwa.
Ameongeza, “Kutofautiana mitazamo, ni jambo la kawaida kwenye siasa. Lakini viongozi wawili wa ngazi ya juu (Rais na Makamu wake), kufikishana mahali kutengenezeana mizengwe hadi mmoja kulazimishwa kujiuzulu, hakuwezi kukubarika.”
Katika hatua nyingine, Mpina amesema, anatarajia kufungua kesi ya kikatiba, kupinga kujiuzulu kwa Dk. Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa Makamo wa Rais na kuteuliwa kwa Deogratius Ndejembi, kushika nafasi yake.
Amesema, ameamua kuchukua hatua hiyo ili kulinda Katiba na utawala wa Kikatiba nchini.
Mwanasiasa huyo amejigamba kwamba amepanga kufungua kesi hiyo mapema iwezekanavyo, ili kuhoji uvunjwaji huo wa Katiba.