SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limefanya mabadiliko ya mwamuzi wa kati atakayechezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba SC ya Tanzania na 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta, baada ya mwamuzi wa awali, Ahmad Imtehaz Heeralall wa Mauritius, kushindwa kusafiri kwenda Tanzania kwa sababu za kifamilia.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, CAF imemteua Amin Mohamed Omar wa Misri kuchukua nafasi ya Heeralall, huku mwamuzi huyo mpya akianza safari ya kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo.
Amin ni miongoni mwa waamuzi wa Afrika waliopata fursa ya kuchezesha mechi za Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Marekani, Canada na Mexico mwaka 2026.
Hata hivyo, mwamuzi huyo ana kumbukumbu isiyopendeza kwa mashabiki wa Simba, baada ya kuchezesha mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara wa msimu wa 2024/2025 kati ya Simba na Yanga, ambapo Simba ilipoteza kwa mabao 2-0.
Kwa mujibu wa ratiba, mchezo huo wa raundi ya pili ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utachezwa Jumatano 21 Oktoba 2026, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Licha ya mchezo huo kufanyika nchini Tanzania, Simba itakuwa timu mgeni kwa mujibu wa taratibu za CAF, huku 15 de Agosto ikiwa mwenyeji wa mchezo huo katika hatua ya kiutawala.
Mwisho.