MADEREVA wa Mabasi yaendayo mikoa mbalimbali nchini wamegoma kuendelea kutoa huduma ya ya usafirishaji kwa madai ya ukamatwaji holela wa gari na kufungiwa kwa leseni zao kinyume cha utaratibu.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Pia madereva hao wanadai baadhi ya askari wa usalama barabarani, wmekuwa wakiweka mawakala katika shughuli za usafirishaji.
Hali hiyo imesababisha mabasi kadhaa kubaki stendi bila kuanza safari kama ilivyopangwa, huku abiria wakisubiri hatma ya safari zao.
Mmoja wa madereva hao amesema kuwa wamekuwa wakiwekewa vikwazo vikali vya kazi kupelekea kufungiwa kwa leseni zao “Hujafika Dar es Salaam tayari ushapata adhabu ya kufungiwa leseni sasa familia zetu zikale wapi”.
Mgomo huo, iwapo utaendelea, unaweza kuathiri usafiri wa abiria wanaotoka Dar es Salaam kwenda mikoa mbalimbali nchini, hasa katika kipindi ambacho stendi hiyo hutumiwa na maelfu ya wasafiri N mgomo huu unausisha mikoa mingine kama mwanza,mbeya,dodoma.
MwanaHALISI Digital inaendelea kufuatilia tukio hilo na itawajuza wasomaji kuhusu hatua zitakazofuata pamoja na msimamo wa madereva na mamlaka zinazohusika.