UPANDE wa serikali kwenye kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), umeiambia Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kuwa mashahidi wa utetezi wameshindwa kumtetea mshtakiwa.Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo yameelezwa leo tarehe 29 Septemba 2026, na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga wakati anafanya majumuisho ya hoja za upande wa mashtaka mbele ya jopo la majaji watu linaloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.
Katuga ameeleza kuwa upande wa utetezi ulifika mahakamani hapo kutoa ushahidi wa utetezi wakiwa hawana wajualo kwenye shauri hilo.
“Waheshimiwa, mtaona upande wa utetezi hawaweza kujitetea hata kidogo, zaidi ya “sijui”, “sikumbuki” kuwa nyingi,” alieleza Katuga.
“Waheshimiwa Majaji, kifungu ambacho tumekirejea cha 3(2)(a) kinataka kuthibitisha beyond reasonable doubt (kuthibitisha bila kuacha shaka),” alidai Katuga.
Mashahidi wa utetezi kwenye kesi hiyo ni pamoja na John Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Mnyika Katibu Mkuu wa chama hicho, Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu na Brenda Rupia Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema.