CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimemtaka Waziri wa mambo ya ndani Patrobas Katambi ajiuzulu nyazifa hiyo kutokana na kadhia ya mgomo wa madereva wa mabasi iliyotokana na uamuzi wa mfumo wa kukata pointi 15 katika leseni zao inayopelekea kungiwa kwa lesini hizo.Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo yamehanikizwa leo tarehe 29 Septemba 2026 na Naggy Kaboyoka, Wairi Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu.
Amesema kuwa Madereva walieleza upungufu wa mfumo huo na utekelezaji wake. “Ni wazi kuwa ni mfumo kandamizi, unaweka mzigo usio wa haki kwa madereva, unaongeza hofu ya kupoteza ajira, na kufungua mianya ya rushwa na uonevu,”amesema Kaboyoka.
Ameongeza kuwa “Serikali haikuchukua hatua na kutafuta suluhu. Badala yake Waziri alieleza kwamba mfumo huo upo kwenye majaribio, wakati madereva wanakumbana na changamoto, vitisho, faini na wengine kufungiwa leseni zao,” ameeleza.
Amesema kuwa matokea ya ushapazaji shingo huo umepelekea kutopatikana kwa huduma ya usafiri .
“Hali hii imeathiri wananchi wanaotegemea usafiri wa barabara kwa ajili ya kwenda hospitalini, kwenye biashara, kusafirisha mizigo na katika shughuli nyingine za kila siku,” .
Kaboyoka amesisitiza kuwa chama hicho kinamtaka Waziri aachie ngazi
“ACT inamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, kujiuzulu mara moja kwa kushindwa kuchukua hatua kwa wakati za kusikiliza malalamiko ya madereva na kuzuia mgogoro huu usifikie hatua ya kuathiri maisha na shughuli za wananchi,” amesema Kaboyoka.