Timu ya wanawake ya Real Madrid wanatarajia kuanza kampeni yao katika hatua ya ligi ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake UEFA kwa kuwakaribisha timu ya wanawake ya Paris Saint-Germain leo Jumanne, Septemba 22, 2026.
Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Alfredo Di Stéfano, Madrid, kuanzia saa 22:00 usiku, ukiwa ni miongoni mwa michezo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa katika siku ya kwanza ya hatua hiyo.
Kwa Real Madrid, mchezo huu unakuja katika kipindi ambacho timu imeanza kuonyesha kiwango kizuri katika ligi ya ndani. Los Blancos wanaingia baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Valencia, huku Felicia Schröder akiendelea kuonyesha uwezo wake wa kufunga mabao. Kocha Pau Quesada anatarajiwa kuwa na chaguo mbalimbali katika kikosi chake, akiwemo Linda Caicedo na Caroline Weir, ambao wanaweza kuwa sehemu muhimu ya mipango ya Real Madrid katika eneo la ushambuliaji.
Hata hivyo, Real Madrid wanakabiliwa na mtihani mkubwa kutokana na ubora na uzoefu wa PSG katika mashindano ya Ulaya. Katika michezo mitano iliyopita kati ya timu hizi, PSG wameshinda mara tatu, Real Madrid mara moja, huku mchezo mmoja ukimalizika kwa sare. Katika kipindi hicho, PSG wamefunga mabao tisa dhidi ya matatu ya Real Madrid, jambo linaloonyesha ushindani uliokuwepo katika michezo yao iliyopita.
Licha ya historia hiyo, Real Madrid wana takwimu wanazoweza kuzitumia kama chanzo cha matumaini. Timu hiyo bado haijawahi kushinda mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa ikiwa nyumbani, hivyo mchezo huu utawapa nafasi ya kubadili rekodi hiyo mbele ya mashabiki wao. Ushindi dhidi ya PSG pia ungekuwa mwanzo muhimu kwa katika hatua ya ligi, hasa kutokana na umuhimu wa kukusanya pointi mapema Real Madrid katika mashindano.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
PSG, kwa upande wao, wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na uzoefu mkubwa wa kushindana katika kiwango cha juu cha soka la wanawake barani Ulaya. Hata hivyo, wamekuwa na changamoto katika michezo yao ya ufunguzi, baada ya kutoshinda mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa katika misimu mitatu iliyopita na kutofunga bao katika michezo hiyo.
Pia, PSG hawajapata ushindi katika mechi saba za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, rekodi ambayo Real Madrid wanaweza kujaribu kuitumia kama sehemu ya maandalizi yao.
Mchezo huu unatarajiwa kuamua zaidi ya pointi tatu kwa sababu zote mbili zinahitaji kuanza hatua ya ligi kwa matokeo mazuri. Real Madrid watajaribu kutumia uwanja wa nyumbani, kasi ya wachezaji wao wa pembeni na uwezo wa Caicedo pamoja na Weir kutengeneza nafasi, wakati PSG watategemea uzoefu wao na uwezo wa kudhibiti mchezo katika vipindi muhimu.
Kwa kuzingatia historia ya timu hizi na takwimu zao za hivi karibuni, mchezo wa Madrid unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kuanzia dakika za mwanzo hadi mwisho.