TANESCO mkoani Morogoro imewataka wateja wake kuacha matumizi ya mita za kizamani na kutumia mita janja za kisasa za kuweka umeme unaoingia moja kwa moja ili kuokoa muda. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).
Akizungumza katika maonesho ya 88 Kanda ya Mashariki Afisa uhusiano wa Tanesco mkoani Morogoro Erick Mandali amesema tayati mita zaidi ya 470 za kisasa zimeshafungwa kwa wateja mkoani Morogoro na kwamba uhamasishaji unaendelea ili kuhakikisha wateja wote wanapata mita mpya ambazo hazina gharama yoyote na kuendana na mabadiliko ya kidijitali yaliyopo.
Amesema jitihada za kupatikana mita janja kumefanywa ili kumsaidia mteja kuingiza umeme na usome papo hapo jambo linalosaidia kuepuka usumbufu mbalimbali unaochelewesha jamii kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
Amesema matumizi ya mita za zamani humfanya mteja kuhangaika kutafuta nyumba yenye umeme ili aingine luku namna zake na wakati mwingine kupanda kwenye madumu au visruli kuwema namba za luku walizonazo na kutishia kuanguka na kuvunjika sehemu ya miili yao.
Pia amesema mita janja ina uwezo wa kumuonesha mteja matumizi yake aliyotumia sambamba na kupata ujumbe mara umeme unapokaribia kuisha ili wanunue.
Aidha ameisistiza jamii kutumia majiko janja ya umeme katika mapishi ambayo hayatumii umeme mwingi huku yakiwa hayatoi moshi na ni rafiki katika kuhifadhi mazingira.