KUFUATIA hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, kukabidhi Shilingi bilioni 300 kwa taasisi saba za kifedha, ikiwemo NBC, kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa fedha kwa wanawake na vijana katika mnyororo wa thamani wa kilimo, NBC imesisitiza utayari wake kutekeleza mpango huo kupitia suluhisho bunifu za kifedha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Katika kilele cha Maonesho ya Nanenane 2026, NBC Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa NBC, Jacob Nangi, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Bw. Theobald Sabi, ilikabidhi malori 13 kwa Vyama Vikuu vya Ushirika vya RUNALI na Lindi Mwambao, na kufikisha jumla ya malori 28 yaliyokabidhiwa kwa vyama vya ushirika, ikiwemo TANECU na KACU.

NBC pia ilikabidhi mkopo wa uboreshaji wa makazi kwa mkulima Emmanuel Nyambi Masanja, mmoja wa wakulima 57 walionufaika na mpango huo. Hafla ya makabidhiano hayo ilishuhudiwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Dk. Benson Ndiege.

“Uwezeshaji huu unaakisi dhamira ya NBC ya kwenda zaidi ya huduma za kawaida za kibenki kwa kutoa suluhisho zinazogusa uzalishaji, mitaji, usafirishaji, masoko na kuboresha maisha na makazi ya wakulima.’’ Alisema Nangi