Msimu mpya wa ligi kuu ya Ureno Primeira Liga unafunguliwa kwa mechi nzito kati ya mabingwa watetezi FC Porto na wageni wao Alverca. Huu utakuwa msimu wa 134 katika historia ya FC Porto na msimu wao wa 92 mfululizo kwenye ligi kuu ya Ureno.
Rekodi inayoonyesha uzito na uthabiti wa klabu hii miongoni mwa vinara wa soka la Ureno. Uwanja wa Dragão utakuwa na hamasa kubwa ya kufungua msimu mbele ya mashabiki wao wenyewe.
Kimbinu, Porto wanatarajiwa kuingia na mfumo wao wa kawaida wa 4-3-3 chini ya Francesco Farioli. Kikosi kinachotarajiwa kuanza ni pamoja na Diogo Costa kwenye kipa, ulinzi wa Alberto Costa, Thiago Silva, Jan Bednarek na Jakub Kiwior, huku kati ya uwanja wakiongozwa na Victor Froholdt, Pablo Rosario na Gabriel Veiga, na mstari wa mbele ukiwa na Pepê pamoja na wachezaji vijana kama Deniz Gül na Oskar Pietuszewski. Hii inaonyesha mchanganyiko mzuri wa wachezaji wenye uzoefu na wachezji wapya wanaosimamiwa na kocha huyu wa Kiitaliano.
Kwa upande wa Alverca, timu hii inaendelea kubeba changamoto za kiulinzi. Klabu hiyo inaingia ikiwa bado inakabiliwa na majeraha ya wachezaji kadhaa muhimu akiwemo Julian MartÃnez, Francisco Chissumba, FabrÃcio Garcia, Tomas Mendes na Sabit Abdulai. Ukosefu huu wa wachezaji muhimu unaweza kuathiri sana uwezo wao wa kupambana na mashambulizi ya Porto, hasa wakizingatia jinsi wanavyocheza mbali na nyumbani kwao.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Historia ya moja kwa moja kati ya timu hizi inaonyesha wazi utawala wa Porto. Katika michezo kumi na mbili ya mwisho, Porto wameshinda mara tisa, Alverca hawajawahi kushinda hata mara moja, na mechi tatu zimeishia sare, huku bao zikiwa 26-5 kwa niaba ya Dragões.
Mchezo wao wa hivi karibuni zaidi msimu uliopita katika uwanja huohuo uliisha kwa ushindi mdogo wa 1-0 kwa Porto, ukionyesha kuwa hata pale Alverca wanapoongeza ulinzi, bado wanashindwa kupata matokeo chanya dhidi ya mabingwa hawa.
Kwa jumla, takwimu zote zinaelekeza kwenye ushindi wa Porto iwe ni kwa historia ya moja kwa moja, ubora wa kikosi, au hali ya majeraha upande wa wageni.
Swali kubwa litakuwa ni kwa tofauti gani Porto watashinda, na kama Alverca wataweza kuonyesha upinzani wowote wa maana katika robo saa za kwanza za mechi kabla ya nguvu ya nyumbani kuwazidi.