RAIA wa China, Zhou Chi (36), ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya TBEA, amehukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita na Mahakama ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutiwa hatiani katika kesi ya shambulio la kudhuru mwili.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro iliyotolewa 25 Juni 2026, Zhou Chi alifikishwa mahakamani 23 Juni 2026 na kushtakiwa katika shauri namba 14154/2026 la shambulio la kudhuru mwili.
Baada ya kusikilizwa kwa shauri hilo, mahakama ilimtia hatiani na kumpa adhabu ya kifungo cha nje cha miezi sita, huku akitakiwa kutotenda kosa lolote la jinai katika kipindi hicho.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi limeweka wazi kuwa mtuhumiwa ni mfanyakazi wa kampuni ya TBEA inayotekeleza mradi wa ujenzi wa laini kuu ya umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma na si mradi wa umeme vijijini REA kama taarifa za awali zilivyoeleza.