Wananchi na mawakala wa meli wamezungumzia fursa mbalimbali zinazotokana na uwekezaji mkubwa wa miundombinu uliofanywa na Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika Bandari ya Mtwara. Anaripoti Mwandishi Wetu……(endelea)
Mizigo inayopakiwa na au kushushwa kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kama Malawi, Zambia, Zimbabwe, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Msumbiji kuongezaka.
Wakizungumza na waandishi wa habari wananchi, mawakala na uongozi wa bandari hiyo wamepongeza uwekezaji huo uliofanywa na Serikali jinsi ulivyofungua fursa kwa kila mmoja.

Mama lishe wa eneo la bandarini, Rehema Mputa, amesema maboresho ya bandari yamebadili biashara yake na kuongeza kipato huku kiongozi wa madereva bodaboda, Issa Mchika akisema shughuli za bandari zimeongeza abiria na kipato kwa madereva.
Wakala wa Meli wa Joyous Shipping Service Ltd, Esthersia Mallya ameeleza mazingira yalivyo rafiki katika bandari hiyo na Kaimu Meneja wa Bandari Mtwara, Hekima Ngeze akielezea maboresho yalivyofanyika na yanayoendelea ili kuifanya kuwa bora zaidi.