WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameelekeza hoteli na nyumba za kufikia wageni nchini kuhakikisha kila mgeni anayefikia katika maeneo hayo anatambulika kwa kutumia kitambulisho kinachokubalika.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama wa wananchi na wageni, pamoja na kurahisisha utambuzi wa watu wanaofikia katika huduma za malazi nchini.
Kwa mujibu wa waziri huyo, wamiliki na wasimamizi wa hoteli pamoja na nyumba za wageni wanapaswa kuhakikisha wanazingatia taratibu za kuhakiki utambulisho wa wageni wote kabla ya kuwapatia huduma za malazi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha usalama na kudhibiti vitendo vya uhalifu.
Aidha, amewataka wadau wa sekta ya malazi kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa pale wanapobaini mgeni mwenye utambulisho unaotia shaka au anayekiuka sheria za nchi.