RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniphace Mwabukusi, amesema Waziri wa Mambo ya Ndani hana mamlaka ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ambayo inaruhusiwa kisheria, akisisitiza kuwa hatua yoyote ya aina hiyo ni kinyume cha Katiba na sheria.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Kupitia taarifa yake, Mwabukusi amesema jukumu la Jeshi la Polisi Tanzania katika mikutano ya ndani ya vyama ni kutoa ulinzi na kuhakikisha usalama, si kutoa vibali au kuzuia mikutano hiyo.
Aidha, amesema TLS imepokea kwa mshtuko taarifa kuhusu maelekezo hayo na inaendelea kutathmini hatua za kisheria itakazoweza kuchukua dhidi ya yeyote atakayetekeleza agizo ambalo imeeleza kuwa ni haramu na batili kwa madai ya kukiuka Katiba na sheria.
Mwabukusi amesisitiza kuwa nchi inapaswa kuongozwa kwa kuzingatia Katiba na sheria, badala ya matamko ya viongozi.