MWANATAALUMA Prof. Issa Shivji amesema taifa lipo katika kipindi cha maombolezo kutokana na kukosekana kwa uwajibikaji kuhusu yaliyotokea Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa hali hiyo inahitaji wananchi kuendelea kushikamana na kutafakari njia za kujenga haki, amani na utawala bora.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza leo 28 Agosti 2026, katika Jukwaa la Demokrasia Tanzania (Tanzania Democracy Forum), Prof. Shivji amesema ni muhimu mazungumzo kuhusu haki ya mpito na mustakabali wa taifa kuendelea, ili kusaidia kupata suluhisho la changamoto zinazolikabili taifa.
“Tuko kwenye maombolezo, lakini tunapaswa kuendelea kusimama pamoja na kutafuta haki na mwelekeo bora wa nchi yetu,” alisema Prof. Shivji