CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kesho Jumamosi 29 Agosti 2026 kitafanya kikao cha Kamati Kuu Maalumu jijini Dar es Salaam.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Kikao hicho kinafanyika ikiwa imepita takribani miezi miwili tangu kikao cha mwisho kilichofanyika mkoani Kigoma 30 Juni 2026.
Katika kikao hicho, Chadema kilitoka na maazimio zaidi ya 10 ikiwemo kuitaka Serikali kushusha gharama za mafuta na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kulipa malimbikizo ya fedha za ruzuku za chama hicho na kuendeleza mapambano ya Katiba mpya.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa Leo Ijumaa 28 Agosti 2026 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema, Brenda Rupia imeeleza kuwa, kikao hicho kitakachofanyika makao makuu ya Chadema, Edwin Mtei House, Mikocheni.