Mahakama ya Wilaya ya Pangani imemhukumu Juma Zakayo Nima, mwenye umri wa miaka 40 na mkazi wa Mtango Village, kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 3.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Akisoma hukumu hiyo tarehe 28 Agosti 2026, Hakimu Magwiza amesema Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka na hivyo kujiridhisha kuwa kosa hilo limethibitishwa dhidi ya mshtakiwa.
Hakimu Magwiza amesema hukumu hiyo imetolewa kwa kuzingatia sheria na kuhakikisha haki inatendeka, huku ikiwa ni fundisho kwa watu wengine wanaoweza kujihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Kwa mujibu wa maelezo ya kesi, mtuhumiwa alifikishwa mahakamani kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 3.
Kesi hiyo yenye Namba CC No. 17946/2026 ilisikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Pangani, ambapo baada ya kusikiliza ushahidi uliowasilishwa, Mahakama ilimkuta Juma Zakayo Nima na hatia.
Mahakama imemhukumu mtuhumiwa huyo kutumikia kifungo cha maisha jela.