DK. Rugemeleza Nshala, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema kuwa Said Issa Mohammed na wenzake watalipa hasara waliyoisababishia Chadema kutokana na kukishtaki chama hicho na kupelekea kuzuia chama hicho kufanya shughuli zake mwaka mzima. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Dk. Nshala amesema kuwa kesi hiyo ilikisababishia Chama hasara ya zaidi ya sh. 100 bilioni hivyo Said Issa, mwenzake watalipa hasara hiyo ‘mwanakulitafuta mwanakulipata’.
Dk. Nshala ameyazungumza hayo nje ya mahakama mara baada ya kuahirishwa kwa maombi mapya ya Said Issa Mohammed ambayo anakusudia kufungua kesi dhidi ya Chadema wakitaka kuzuiwe kufanya shughuli za siasa .
Dk. Nshala amesema kuwa shauri hilo litatajwa tarehe 6 Julai na kabla tarehe 2 Julai chama hicho kimetakiwa kujibu kiapo kinzani.
Hata hivyo Chadema imeweka wazi kuwa tayari Chama hicho kishakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Jaji Ngunyale wa kuondoa kesi ile ya awali .