NAIBU Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Amani Golugwa, ametoa wito kwa Jeshi la Polisi Tanzania kumkamata Sheikh Mwaipopo ndani ya saa 72 kutokana na madai kwamba ana kikundi kinachoitwa “Mbwa Mwitu” ambacho kinadaiwa kujiandaa kufanya vitendo vya uhalifu.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Akizungumza kuhusu suala hilo, Golugwa alilitaka Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa Camillus Wambura kuchukua hatua za haraka kuchunguza madai hayo na kuhakikisha sheria inafuatwa.
Golugwa alisema kuwa iwapo taarifa hizo ni za kweli, mamlaka husika zinapaswa kuchukua hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi ili kuzuia vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa wananchi na mali zao.