RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amerejea nchini leo 6 Juni 2026, akitokea St. Petersburg, Urusi alikohitimisha ziara ya kitaifa ya siku tatu.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais Samia alipokelewa na Makamu wa Rais, Balozi Emmanuel John Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Asha-Rose Migiro.
Ziara hiyo ilifanyika kufuatia mwaliko wa Rais wa Shirikisho la Urusi,Vladimir Putin, na ililenga kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika sekta za biashara na uwekezaji, elimu, sayansi na teknolojia, nishati, madini, kilimo na miundombinu.
Wakati wa ziara hiyo, Rais Samia alitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha RUDN, sambamba na kufungua fursa mpya za ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi kwa manufaa ya pande zote mbili.