LEO Juni 5, 2026 saa 13:00 kwa saa za Afrika Mashariki (saa 18:00 GMT), Uwanja wa Stade El Bachir mjini Mohammedia, Morocco utakuwa jukwaa la mchezo wa kirafiki kati ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na Togo.
Mechi hii ni sehemu ya maandalizi ya timu zote mbili kwa ajili ya kufuzu kwa AFCON 2027 itakayoanza Septemba 2026. Uwanja uliobadilishwa kutoka Rabat hadi Mohammedia unatarajia kuwa na hali ya hewa ya wastani kwa ajili ya soka.
Katika historia timu hizi zimekutana mara moja tu, Togo wakishinda mechi hiyo pekee. Kwa upande wa Togo, wana rekodi nzuri ya kutofungwa katika mechi zao za ugenini hivi karibuni, huku Jamhuri ya Afrika ya Kati wakijulikana kwa mchezo wa kukaba na nguvu za kimwili. Katika mechi za kirafiki za mwaka 2026, Togo wana asilimia 50 ya ushindi huku CAR wakiwa bado hawajashinda mechi yoyote.
Kocha wa Togo Dare Nibombe ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kinachojumuisha wachezaji wapya watano. Miongoni mwa nyota wanaotarajiwa ni mshambuliaji Kevin Denkey (FC Cincinnati, USA) na Kodjo Fodoh Laba (Al Ain, UAE) ambao ndio chaguo la msingi la ushambuliaji. Wachezaji wapya kama Bastou Djibril, ambaye amekuwa akivutia katika klabu yake ya AS Gbohloe-Su, wanatazamiwa kupata fursa ya kujithibitisha katika mechi hii.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Jamhuri ya Afrika ya Kati inaweza kukosa baadhi ya wachezaji wao wakuu kutokana na majeruhi na uchovu wa safari. Katika mechi zao za awali za kufuzu Kombe la Dunia, waliweza kuwa na wachezaji kama Geoffrey Kondogbia, Louis Mafouta na Isaac Koyalipou katika safu ya ushambuliaji. Timu hii inategemea sana nguvu za mwili na mipira mirefu kuvunja ulinzi wa Togo.
Kutokana na timu zote kuwa katika mchakato wa kujenga na kuepuka majeruhi. Mechi ya pili ya Togo itakuwa dhidi ya Benin Juni 9, hivyo Kocha Dare Nibombe atatumia mechi hii kuwapa dakika wachezaji wapya na kukata orodha ya wachezaji wa kudumu.