Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza,
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa ambazo zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Chama cha Mapinduzi (CCM) kuigomea Ofisi hiyo. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Hatua hiyo imekuja baada ya Ofisi ya Msajili nchini kuiandikia barua rasmi Chama cha Mapinduzi (CCM), ikikitaka kutoa maelezo na ufafanuzi wa kina kufuatia kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, inayodaiwa kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa.
Kwa mujibu wa Afisa katika Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza, Ofisi ya Msajili ilikipa chama hicho ukomo wa hadi 29 Mei 2026, kuandika maelezo yake rasmi ambapo tayari imewasilisha majibu ya barua hizo 19 Mei 2026 katika Ofisi ya Msajili.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, ametoa ufafanuzi huo leo tarehe 1 Juni 2026 na kudai taarifa hiyo ya CCM kuigomea Ofisi hiyo zipuuzwe