RAIS wa Senegal, Bassirou Faye ametangaza baraza jipya la mawaziri, ikiwa ni wiki moja tu tangu alipomteua Ahmadou Al Aminou Lo kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Mabadiliko hayo yametangazwa jana 1 Juni 2026, baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Ousmane Sonko kuondolewa madarakani.
Sonko ametangaza kuwa chama chake cha Pastef hakitashiriki katika kuunda serikali mpya, jambo linalotafsiriwa kama ishara ya kuendelea kwa mvutano wa kisiasa ndani ya utawala huo.
Baraza jipya la mawaziri lililotangazwa na Rais Faye linatarajiwa kuanza kazi mara moja baada ya uteuzi huo licha ya Chama cha Pastef kujiondoa.