IRAN na Israel zimetangaza kusitisha mapigano kufuatia mwito wa Rais wa Marekani, Donald Trump, huku Iran ikionya kuwa hatua hiyo inaweza kuvunjika iwapo Israel itaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya Lebanon.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Mvutano kati ya pande hizo mbili uliongezeka baada ya Iran kurusha makombora kuelekea maeneo ya kaskazini mwa Israel, ikidai ilikuwa ikijibu mashambulizi ya Israel dhidi ya mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Israel nayo ilijibu kwa kufanya mashambulizi katika miji kadhaa ya Iran, ikiwemo Tehran, na kusisitiza kuwa iko tayari kuchukua hatua zaidi endapo usalama wake utatishiwa.
Mapigano hayo yalisababisha kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kwa takriban asilimia 5, huku yakiongeza hofu kuhusu upatikanaji wa nishati duniani. Wasiwasi huo umeendelea kuongezeka tangu mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya Iran na Marekani pamoja na Israel mapema mwaka huu.