RAIS Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amekutana na Rais wa Kenya, William Samoei Ruto, katika mkutano wa kimataifa wa Oslo Forum 2026 unaofanyika mjini Oslo, nchini Norway tarehe 10 hadi 11 Juni 2026. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mkutano huo wa kila mwaka unawakutanisha wasuluhishi wa migogoro, viongozi wa ngazi za juu pamoja na wataalamu wa masuala ya amani kutoka zaidi ya nchi 50 duniani kwa lengo la kujadili namna bora ya kuimarisha amani na kutatua migogoro inayozikumba jamii mbalimbali.
Mwaka huu, jukwaa hilo linafanyika chini ya kaulimbiu isemayo “The Cost of War, the Price of Peace” (Gharama ya Vita, Thamani ya Amani), ikisisitiza umuhimu wa kutafuta suluhu za amani huku dunia ikikabiliwa na changamoto mbalimbali za migogoro na vita.