SERIKALI ya Malawi imetangaza kuwa itaungana na nchi nyingine katika mpango wa kuwarejesha nyumbani raia wake walioko Afrika Kusini ambao wameomba msaada kufuatia mashambulizi dhidi ya wahamiaji yanayoendelea kushuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Kupitia taarifa iliyotolewa Jumanne na Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, serikali imeeleza kuwa mpango huo utawahusu raia walioomba kurejeshwa pekee, huku ikibainisha kuwa maelezo zaidi kuhusu utekelezaji wake yatatolewa baada ya taratibu zote kukamilika.
Afrika Kusini imekuwa ikikabiliwa na matukio ya mara kwa mara ya mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni, ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakiwalaumu wahamiaji kwa kuchukua ajira na fursa za kiuchumi zinazodaiwa kuwastahili raia wa nchi hiyo.
Serikali na wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa wito wa kukomeshwa kwa vitendo hivyo na kulinda haki za wahamiaji wote.