MAKAMU wa Rais wa Tanzania,Balozi Emmanuel Nchimbi ametembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kilele cha Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani 2026 yanayofanyika jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Balozi Nchimbi ametembelea banda la REA leo 5 Juni 2026 ambapo ameelezwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Wakala maeneo ya Vijijini na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala Advera Mwijage.
Mwijage amemueleza Balozi Nchimbi kuwa, kupitia miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imesaidia kupunguza athari za uharibifu na uchafuzi wa mazingira.
Maonesho ya mwaka huu yamepambwa na kauli mbiu isemayo: Dira 2050 Tuwajibike Kukijanisha Tanzania