RAIS wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi ametangaza kuwa Jumatano 17 Juni 2026, itakuwa siku ya mapumziko rasmi Zanzibar kwa ajili ya kusherehekea Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1448 Hijria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Mwinyi ametoa tamko hilo leo 15 Juni 2026,Ikulu Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Seriklai wa kuutambua Mwaka Mpya wa Kiislam kuwa miongoni mwa siku muhimu Zanzibar
Tangazo hilo limetolewa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislamu, unaoanza mwezi wa Muharram, ambao ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya Hijria.
Serikali imewataka wananchi kutumia siku hiyo kwa amani, mshikamano na kushiriki shughuli mbalimbali za kidini na kijamii zinazohusiana na maadhimisho hayo.