MAKAMU Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, leo 3 Juni 2026 ameendelea na zoezi la kupandisha bendera za chama katika vizimba mbalimbali vya Chadema eneo la Kilwa Kivinje, mkoani Lindi.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Katika shughuli hiyo, Heche ameambatana na Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini, Belchomas Ponera, ambaye ni mwenyeji wake katika ziara hiyo.
Mbali na zoezi la kuimarisha uwepo wa chama katika maeneo mbalimbali, Heche anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika leo katika mji wa Kilwa Kivinje, ambapo atazungumza na wananchi na wanachama wa Chadema kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa na maendeleo ya chama.