MAKAMU Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, amekishambulia vikali chama tawala cha CCM akikituhumu kwa kulea na kufuga lugha za kibaguzi zinazotolewa na baadhi ya mawaziri wa Zanzibar dhidi ya Watanzania wa Bara.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Akizungumza kupitia Kituo cha Redio cha Nuru FM mkoani Iringa leo Jumamosi, 13 Juni 2026, Heche amezitaja kauli za hivi karibuni za Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Saada Mkuya Salum, na Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji, Hassan Khamis Hafidh, kama matusi yanayohatarisha ustawi wa nchi, huku akisisitiza kuwa suluhu pekee ya kukomesha “uchafu” huo ni kuwepo kwa mfumo wa Serikali Tatu.
Heche amemnyooshea kidole Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kukaa kimya mbele ya kauli hizo, akidai kuwa kama maneno hayo yasingetoka kwenye vinywa vya viongozi wa CCM bali yangesemwa na mwanachama wa Chadema, chama hicho kingekuwa kimeshalimwa barua ya adhabu haraka sana.