WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasilisha ujumbe maalumu wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres na kusisitiza dhamira ya Tanzania ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, amani na maendeleo endelevu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Baada ya mazungumzo yao, Balozi Kombo alimkabidhi Guterres zawadi ya kitabu kuhusu Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutambua kuvutiwa kwa muda mrefu kwa katibu mkuu huyo na maono, uongozi na mchango wa Mwalimu Nyerere katika kuhimiza amani, maendeleo na ushirikiano wa kimataifa.