Boniface Jacob
MWENYEKITI wa Chadema kanda ya Pwani na mjumbe wa kamati Kuu ya Chama hicho Boniface Jacob, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka kuhojiwa jeshi la Polisi Kinondoni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Boni amesema kuwa, amefika kituoni hapo mara baada ya kupokea wito kutoka ofisi ya RCO Kinondoni siku ya jana, na kumtaka afike kituoni hapo siku ya leo tarehe 16 Juni 2026.
Katika mahojiano yao Boni alisema kuwa, Polisi walimuhoji kuhusu tuhuma mbalimbali za kupanga njama za maandamano ya tarehe 7 mwezi ujao, jambo ambalo alisema ni uzushi na hakukuwa na ushahidi wowote kuhusu tuhuma hizo.