NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Ameir amesema kuwa Serikali kupitia Baraza la Mitihani la Tanzania ilifanya utafiti mwaka 2025 na kubaini kuwa sababu zinazowafanya baadhi ya wanafunzi kuandika lugha zisizo na staha kwenye karatasi za mitihani ni pamoja na mmomonyoko wa maadili, msongo wa mawazo pamoja na kukata tamaa kitaaluma.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea)
Amesema matokeo ya utafiti huo yameonesha umuhimu wa kuimarishwa kwa malezi, ushauri nasaha na mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi ili kusaidia kupunguza changamoto hizo.
Aidha, alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa elimu kuhakikisha maadili na nidhamu vinaimarishwa shuleni sambamba na kuwasaidia wanafunzi kukabiliana na changamoto za kisaikolojia na kitaaluma.