SAKATA la mirathi ya aliyekuwa Kiongozi wa Klabu ya Simba na mfanyabiashara maarufu marehemu Zakaria Hanspope limeendelea kuzua mjadala mkubwa baada ya benki moja kudai deni la zaidi ya shilingi bilioni 7 na kutaka kuuza magari zaidi ya 70 yaliyopo katika eneo la Mbezi Jogoo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, zoezi hilo lilisimamishwa na Jeshi la Polisi huku sintofahamu ikiendelea kutawala kuhusu uhalali wa deni hilo.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Familia ya marehemu Hanspope sasa imevunja ukimya na kueleza kuwa deni linalodaiwa na benki hiyo linadaiwa kuchukuliwa mwaka 2024 wakati marehemu alifariki tangu mwaka 2021.

Mrithi wa familia hiyo ambaye ni mtoto wa Marehemu Abel Zacharia Hanspope amedai watu wanaotambulika kwenye mirathi hawakuhusika kwa namna yoyote katika mkopo huo, jambo linaloibua maswali mazito kuhusu nani aliyekopa fedha hizo kwa jina la marehemu.