RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo 19 Mei 2026 ameondoka Nchini kuelekea Kigali, Rwanda kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia Barani Afrika (NEISA).Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es salaam, Rais Samia ameagana na Viongozi mbalimbali waliompeleka Uwanjani kwa ajili ya safari hiyo muhimu ya Kikazi.
Mkutano huo wa kimataifa unawakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali, Wataalamu wa nishati, Wawekezaji pamoja na mashirika ya Kimataifa kujadili matumizi ya nishati ya Nyuklia katika kuchochea maendeleo ya Bara la Afrika.
Aidha, mkutano huo unatarajiwa kujadili njia bora za kuongeza upatikanaji wa umeme Afrika, kupunguza uchafuzi wa mazingira, kusaidia maendeleo ya viwanda, kukuza ubunifu wa teknolojia za nishati ya Nyuklia pamoja na kuvutia wawekezaji katika miradi mbalimbali ya nishati Barani Afrika