MKAZI wa Kisaba, Mlandizi wilayani Kibaha, Ramadhan Iddi Feli mwenye umri wa miaka 27 amehukumiwa kifungo cha miaka 37 jela na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha baada ya kutiwa hatiani kwa kumbaka na kumjeruhi mwanafunzi wa miaka 15 anayesoma kidato cha pili.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Akitoa hukumu18 Mei 2026, Hakimu Mkazi Mfawidhi Emmaeli Lukumai alisema mahakama ilijiridhisha na ushahidi uliowasilishwa kuwa mshtakiwa alimvamia mwanafunzi huyo 10 Machi 102025 katika eneo la Kongo-Soga akiwa njiani kwenda shule, kisha kumjeruhi na kutekeleza kitendo hicho cha kinyama.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani lilimkamata mtuhumiwa siku mbili baada ya tukio kuripotiwa Kituo cha Polisi Mlandizi na kuanza uchunguzi uliosababisha kufikishwa mahakamani.
Mahakama ilimpa miaka 30 jela kwa kosa la ubakaji na miaka saba kwa kosa la kujeruhi, pamoja na kuamuru alipe fidia ya jumla ya Sh milioni 1.5 kwa manusura huyo.