JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza kifo cha mfanyabiashara Bhaozang Ge, aliyepoteza maisha usiku wa tarehe 16 Mei 2026 eneo la Mabibo, Wilaya ya Ubungo.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Kulingana na taarifa rasmi iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, marehemu mwenye umri wa miaka 50, alikuwa mmiliki wa Kiwanda cha Chupa Xil Li kilichopo Mabibo.
Taarifa inaeleza kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 8:00 usiku, ambapo marehemu alishambuliwa na walinzi binafsi wa kiwanda chake, jambo lililosababisha kifo chake papo hapo.
Jeshi la Polisi limebainisha kuwa upelelezi wa kina unaendelea ili kubaini sababu halisi ya tukio hilo na kuwafikisha watuhumiwa mbele ya sheria.
Kamanda wa Polisi amehakikishia umma kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika wote watakaobainika kuhusika na mauaji hayo.