JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia Kitengo cha Kuzuia Makosa Yanayohusiana na Fedha (FCU), linawashikilia watu saba akiwemo raia mmoja wa China kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa njia ya mtandao wa fedha zinazokadiriwa kufikia Shilingi Bilioni 2.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
​Taarifa rasmi iliyotolewa leo 21 Septemba 2026, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, imewataja baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Steven Deogratius Mganga pamoja na raia wa China aitwaye Zhi Hang Wang.
​Jeshi la Polisi limebainisha kuwa mtandao huo unadaiwa kutekeleza matukio hayo ya wizi wa mtandao katika mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Dodoma, na Tabora.
“Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha FCU limewakamata watuhumiwa 7 akiwemo Steven Deogratius Mganga na raia mmoja wa China aitwaye Zhi HANG WANG kwa tuhuma za wizi kwa njia ya mtandao wa pesa zinazokadiriwa kuwa kiasi cha shilingi bilioni mbili, matukio ambayo yanadaiwa kutekelezwa katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Tabora. Taratibu zaidi za kisheria zinaendelea,” imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa na SACP Muliro.
​Jeshi hilo limeeleza kuwa hatua zaidi za kisheria na upelelezi vinaendelea kabla ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani.