JOHN Pambalu, Mkurugenzi wa Organizesheni na Uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameshtakiwa na Jamhuri kwa tuhuma za uhaini.Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Pambalu amshtakiwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo tarehe 21 Oktoba.
Katika mashtaka yake anadaiwa kati ya tarehe 1 Septemba 2025 na tarehe 29 Oktoba 2025 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, kufanya ushawishi wa kuvuruga uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Katika mashtaka hayo Pambalu anadaiwa kuitisha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pambalu ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa chama hicho (Bavicha) kwa kipindi cha miaka sita (2019-2025).
Mwisho.