SERIKALI imetumia zaidi ya Sh. 4.4 bilioni kuboresha huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Uwekezaji huo unaolenga kupunguza adha ya wananchi kusafiri kilomita 120 kwenda Songea kutafuta huduma za matibabu za ngazi ya juu.
Akizungumzia uwekezaji huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Samson Sanga, amewataka wananchi kutumia kikamilifu huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo ambapo sasa inatoa huduma zilizokuwa zikipatikana nje ya Madaba.
Amebainisha kuwaMaboresho hayo yameimarisha upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu, zikiwemo X-ray, ultrasound, maabara na upasuaji, hatua inayoongeza uwezo wa wananchi kupata huduma karibu na maeneo yao.
Anastasia Komba, mkazi wa Madaba, ni miongoni mwa wananchi wanaonufaika na maboresho hayo amepongeza jitihada zilizofanywa na Serikali.
Ameeleza kuwa upatikanaji wa huduma karibu na makazi yao unaweza kupunguza muda wa safari na gharama zinazohusiana na matibabu hasa kwa wagonjwa wanaohitaji uchunguzi na ufuatiliaji wa mara kwa mara.
Kwa upande wa utoaji wa huduma, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Madaba, Dk. Dickson Mero, na Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Filbert Manyilizu, wameeleza kuwa maboresho ya miundombinu na vifaa tiba huchochea kuimarika kwa huduma zitolewazo kwa wagonjwa.
Mwisho.