KLABU ya Simba SC, imetangaza rasmi kuwa mashabiki wake wameruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya 15 de Agosto, utakaochezwa kesho, Jumatano 21 Oktoba 2026, katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa iliyotolewa leo, 20 Oktoba 2026 na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, imesema ruhusa hiyo imepatikana baada ya mazungumzo ya kina kati ya uongozi wa klabu hiyo na wapinzani wao wa 15 de Agosto, ambao hatimaye wamekubali ombi la kuruhusu mashabiki kuhudhuria mchezo huo.
Simba imeeleza kuwa ilifanya juhudi kubwa kuhakikisha mashabiki wanapata nafasi ya kuingia uwanjani kutokana na umuhimu wao katika kuongeza hamasa na nguvu kwa wachezaji wakati wa mchezo.
Aidha, klabu hiyo imetangaza kuwa mchezo huo utaonyeshwa kupitia skrini kubwa (Big Screen) katika maeneo ya Mwembeyanga na Mbagala Zakheim, jijini Dar es Salaam, ili kuwapa mashabiki wengine fursa ya kufuatilia mchezo huo ambao awali ilitangazwa kwamba ungechezwa bila mashabiki.
Mwisho.