MADAKTARI nchini Kenya wameiwekea serikali saa 48 kutoa ufafanuzi kuhusu mazungumzo yanayoendelea kati yake na Marekani juu ya mpango wa kujenga karantini ya kuwaweka raia wa Marekani wanaoshukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Watoa huduma hao wa afya wameonya kuwa wataitisha mgomo wa kitaifa ikiwa serikali itaendelea na mpango huo bila kuwepo kwa uwazi wa kutosha pamoja na maboresho katika sekta ya afya nchini humo.
Wakati huo huo, Mahakama Kuu ya Kenya imesitisha kwa muda ujenzi wa karantini hiyo kufuatia shauri lililowasilishwa mahakamani kupinga utekelezaji wa mpango huo.
Mahakama hiyo pia imeagiza serikali kutompokea mtu yeyote anayeshukiwa kuambukizwa ugonjwa wa Ebola hadi pale shauri hilo litakapopatiwa uamuzi wa mwisho.