MAKAMU wa Rais wa Tanzania Emmanuel Nchimbi amewasili katika Viwanja vya Kilimani Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita kwa ajili ya kushiriki Ibada ya kumuaga na kumuombea Marehemu Suzana Ngolo Magufuli.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Ibada hiyo inayofanyika leo 29 Mei 2026 imewakutanisha viongozi mbalimbali wa Serikali, dini pamoja na wananchi waliojitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli.
Mamia ya waombolezaji wameendelea kufurika katika Viwanja vya Kilimani, Chato, kuungana na familia, ndugu na marafiki katika kipindi hiki cha maombolezo ya Marehemu Suzana Ngolo Magufuli.