SERIKALI ya Marekani imeipatia Kenya dola za Kimarekani milioni 13.5 sawa na takribani shilingi za Kitanzania bilioni 35.5 kwa ajili ya ujenzi wa kituo maalum cha karantini kitakachotumika kuwaweka raia wa Marekani wanaoshukiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Ebola.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ….(endelea).
Marekani imeeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha ulinzi wa afya na usalama wa raia wake, kwa kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini humo kupitia wasafiri wanaotoka maeneo yenye hatari ya maambukizi.
Mradi huo unatajwa kuwa sehemu ya mikakati ya maandalizi ya dharura dhidi ya milipuko ya magonjwa hatari duniani, huku Kenya ikichaguliwa kutokana na nafasi yake ya kimkakati katika ukanda wa Afrika Mashariki.