KAMATI ya Maafa Wilaya ya Magu imewataka wananchi wachukue tahadhari na kudumisha usafi wa mazingira ili wajikinge na magonjwa ya mlipuko na mvua za El Nino.Anaripoti mwandishi wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kamati hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuchukua tahadhari dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mvua za El Niño.
Kamati hiyo, ikiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Magu, Zuberi Said Zuberi, pamoja na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, jana Oktoba 9, 2026, imefanya ziara ya kukagua maeneo hatarishi katika kata za Kongolo, Chabula na Nyanguge.
Katika ziara hiyo, wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari na kudumisha usafi wa mazingira ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko, hususan wakazi wa Kisiwa cha Kishoka kilichopo Kata ya Chabula.
Mwisho.