KESI ya Katibu wa Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami, na wenzake 16 wanaokabiliwa na mashtaka ya ugaidi, imeahirishwa hadi 25 Septemba 2026.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Kesi hiyo imeahirishwa baada ya upande wa Serikali kueleza kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo kushindwa kuendelea na hatua inayofuata ya kesi.
Mnyawami na wenzake 16 wanakabiliwa na mashtaka hayo baada ya kukamatwa katika vipindi tofauti vya mwezi Juni na Julai 2026.
Katika mwenendo wa kesi hiyo, upande wa Serikali umeendelea kuomba muda zaidi kwa ajili ya kukamilisha upelelezi, huku watuhumiwa wakisubiri hatua zaidi za kisheria.
Mahakama imepanga kesi hiyo kutajwa tena 25 Septemba 2026, ambapo upande wa Serikali unatarajiwa kutoa taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa katika upelelezi wa shauri hilo.
Kwa mujibu wa taratibu za kisheria, watuhumiwa hao wanaendelea kuchukuliwa kuwa hawana hatia hadi pale itakapothibitika vinginevyo na mahakama yenye mamlaka.