MAHAKAMA ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, tarehe 9 Septemba 2026, imemhukumu Hiari Juma Salumu kifungo cha miaka thelathini (30) jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya.Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Hukumu hiyo katika kesi namba 20238/2026 imetolewa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa Jonas Lyakundi, baada ya mshtakiwa kufikishwa mahakamani tarehe 8 Septemba 2026 na kusomewa shtaka lake, ambapo alikiri kosa. Upande wa Jamhuri katika shauri hilo uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali John Remmy na Upendo Mgaya.
Kwa mujibu wa taarifa ya tukio hilo, mnamo tarehe 2 Agosti 2026 katika eneo la Kijiji cha Litama, Wilaya ya Ruangwaâ…˜ mkoani Lindi, Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinani wilaya yal Ruangwa , Mrakibu msaidizi wa polisi Frank Mapunda, akiwa katika doria na askarif wenzake, alipata taarifa kwamba mshtakiwa alikuwa akijihusisha na biashara ya kuuza bangi nyumbani kwake.
Baada ya kupata taarifa hizo,Mkuu huyo wa upelelezi Mrakibu msaidizi wa polisi Frank Mapunda kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Litama, Kizito Adrian Chikomele, walifanya upekuzi ndani ya nyumba ya mshtakiwa na kufanikiwa kukamata bangi yenye uzito wa gramu 56.75.
Mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani, ambapo alikiri kosa hilo na shauri hilo liliahirishwa hadi tarehe Septemba 9,2026 kwa ajili ya kutolewa kwa hukumu.